BWANA, WEWE UNANITOSHA

Gary Wilkerson

"Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lillilo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; amabaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili" (1 Wakorintho 10:13).

Paulo anaandika kwa Wakorintho na anawahakikishia. "Wewe uko tayari kuanguka? Unajisikia kama huwezi kuendelea? Naam, kuhimizwa kwa sababu nina neno jema kwako. Watu wengi wamepitia katika majaribu kama hayo unayopitia, lakini hawajafanikiwa!" Kwa nini? Kwa sababu Mungu ni mwaminifu na atatoa njia ya kutorokea.

Mungu ni mwaminifu! Wale walio karibu nawe wanaweza kuwa waaminifu; Kwa kweli, mimi si mwaminifu kwa nguvu zangu. Lakini Yesu anaishi ndani yetu na haki ya Mungu inafanyika katika maisha yetu.

Unapokutana na Yesu, mbegu ya Mungu inakaa ndani yako. Damu ya Mwana-Kondoo aliotolewa kama dhabihu msalabani inakuwezesha wewe na mwili wako, akili, moyo na roho hubadilishwa. Yesu huchukua moyo wako na kukugeuza, na kukufanya kiumbe kipya.

Mungu atatoa njia ya kukimbilia! Utamaduni wetu hutoa njia nyingi za kukimbia lakini Neno la Mungu linasema kwamba Yesu ndiye njia ya kukimbilia. Mungu atatoa! Kumbuka Ibrahimu alipopanda mlima ili kutoa mwanawe mwenyewe kama dhabihu. Alikuwa akienda kwa nguvu zake mwenyewe lakini Mungu alimzuia na kusema, "Sio mwili wako, Ibrahimu. Mimi nitakupa sadaka kwa ajili yako" (angalia Mwanzo 22:12-13).

Haijalishi nini unakabiliwa leo, unaweza kumwamini Mungu kukupa njia ya kutokea - njia ya kukimbilia. Mtazameni na ukiri, "Bwana, wewe unanitosha. Kwa neema yako ninaweza kushinda kila jaribu katika maisha yangu: kukata tamaa, hofu, hasira, tamaa, nguvu yoyote ya giza ambayo inakuja dhidi yangu."