BWANA HUPENDA KANISA LAKE

David Wilkerson (1931-2011)

Ayubu anauliza, "Je! Mtu ni nini, hata ukamtukuza, na kumtia moyoni mwako, na kumwangalia kila asubuhi na kumjaribu kila wakati?" (Ayubu 7:17-18).

Waebrania 12:1 inatuambia kwamba ulimwengu umezungukwa na wingu la mashahidi ambao wako pamoja na Kristo katika utukufu. Je! Hii wingu kubwa inashuhudia - na ushahidi wao una maanniisha ? Wanaongea na kizazi chetu, kupitia maisha yao na maneno yao kama ilivyoandikwa katika Maandiko. Ninaamini wanasema mambo matatu kwetu:

  1. Wao ni mashahidi wa kwamba moyo wa Mungu bado umewekwa juu ya kuokoa dunia hii iliyopotea. Mungu bado anaendelea kutenda kazi, akimimina Roho wake juu ya mwili wote na kuhamasisha wanaume na wanawake katika kila taifa.
  2. Moyo wa Mungu bado umewekwa kwa upendo na kuhifadhi kanisa lake. Hata kwa uasi na kuludi nyuma, Bwana hupenda sana Mwili wake.
  3. Moyo wa Mungu bado umewekwa juu ya kila mtoto wake. Bwana hata achia nyuma yake mtumishi japo ni mmoja. Andiko linatuambia, "Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio na masikio yake husikiliza maombi yao" (1 Petro 3:12).masikio yake husikiliza maombi yao.

Mtume Petro ni umoja kati ya wingu hili la mashahidi na anaelewa kwa nini Mungu ana subira sana. Amlani Yesu, akiapa kwamba hakuwahi kumjua. Petro anataka kusema kwamba Mungu anachikilia hukumu yake juu ya kizazi hiki, ingawa kuna watu wengi ambao bado wanamlaani na kumkana, kama alivyofanya.

Mtume Paulo pia ni mmoja kati ya wingu hili la mashahidi na anawashuhudia upendo wa Mungu usio na kikomo. Paulo alilaani jina la Kristo - alikuwa ni gaidi, mwenye kuwinda watu wa Mungu na kuwasukumia kwa kufungwa au kuuawa. Lakini alikuwa akifanya hayo yote kwa ujinga. Paulo anataka kusema kwamba Mungu ana subira kwa kizazi hiki kwa sababu kuna wengi ambao hufanya dhambi kwa ujinga, kama vile alivyofanya. Hajawahi kuhubiriwa ujumbe wa injili.

Angalia uhakikisho wa kujua kwamba macho ya Mungu huwa juu yetu na moyo wake umewekwa kwa kupenda kila mtoto wake.