BWANA ANAFIKISHA NENO LAKE

David Wilkerson (1931-2011)

Sijawahi kujisikia kukosa wusaidizi na wasiwasi zaidi kuliko wakati tulirudi New York City kuanza Kanisa la Mraba wa Kati (Times Square Church). Mara nyingine tena tulikuwa na rehema ya ratiba ya wamiliki wa nyumba na wakuu wa majengo. Nilipokuwa nahitija kusubiri, si kukuwa na subila kabisa na nililia, "Bwana, kuna mengi ya kufanyika huko New York na wakati mdogo sana. Tunapaswa kusubiri muda gani?"

Lakini mara kwa mara Mungu alinijibu kwa uvumilivu, "Daudi, unaniamini? Ebu ngojea."

Umesikia maneno hayo, "Sehemu ngumu zaidi ya imani ni nusu saa ya mwisho." Ninaweza kushuhudia kutoka miaka yangu katika huduma kwamba kipindi cha kujaribu zaidi daima tu kabla ya Mungu kufanya kazi ya ukombozi wake.

Kuna madhara makubwa wakati hatuwezi kusubiri Mungu atende. Kwa kweli, mara nyingi kwenye muda kama huo tunamshtaki Mungu kwa kutokujali. Sauli alifanya hivyo wakati arikosa subira akaamuwa mwenyewe (tazama 1 Samweli 13). Alikuwa akisema, kwa kweli, "Mungu alinituma kwenda kufanya kazi yake lakini sasa ameniacha kujua jinsi ya kufanya yote ili atimizwe. Mambo yanapoteza udhibiti na hivi karibuni hayatakuwa na matumaini."

 Hii inaelezea mawazo yako wakati mwingine? Tumeamriwa kumngojea Bwana na kumuamini yeye kufanya kazi ya ukombozi wetu. Lakini wakati wa mwisho wetu wa ndani unapoisha, tunakua na hasira kwa Mungu na kujipiga wenyewe. Kwa kumupita mbele yake tunasema, "Mungu hajali mambo yangu. Sala na kusubiri haifanyi kazi. Neno lake haliwezi kutegemea.”

Hata hivyo Mungu ametupa wajibu wa kumusubiri kwa sala. Mwamini na kusema, "Bwana anafikisha neno lake, kwa hivyo mimi sitakua na hofu Mungu ameniambia kusubiri mwongozo wake - na nitangojea. Aca Mungu awe wa kweli na kila mtu ni mwongo!" Katika majaribio yetu, hebu tupatikane na hali hiyo ya moyo. Si kwa hofu, lakini kwa uaminifu!