BILA MTU WA KATIKATI

David Wilkerson (1931-2011)

Wakristo wengi wanataka kusikia na kujua sauti ya Mungu na kwa hakika Mungu anataka kuzungumza na watu wake. Lakini waumini wengi waligeuza kuwa sanamu – wa tumishi wanaoeshimika, mwalimu au minjilisti - ambaye anaongea mambo mema tu kwao. Ili kujua sauti ya Baba, mtu lazima aende moja kwa moja kwake bila mtu wa kati.

Mungu anataka kuzungumza na wewe kama wewe ulikuwa umeketi chakula cha jioni pamoja naye. Anataka kuzungumza na moyo wako kwa moyo, juu ya mambo yoyote na yote. Biblia inasema, "Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akisikia sauti yangu, na kufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami "(Ufunuo 3:20).

Aya hii mara nyingi inatumiwa kwa wasiookolewa; tunasema juu ya Yesu amesimama kwenye mlango wa moyo wa mwenye dhambi, akitaka kuingia. Lakini Kristo anaongea na mwamini! Mstari unaonyesha kwamba anazungumza na wale waliovaa nguo nyeupe (haki), ambao wameinunua dhahabu iliyosafishwa katika moto, ambao macho yao ni mafuta (wana ufunuo), na wanapendwa, wakataliwa na kuwaadhibiwa (tazama mistari 18-19). Hawa ni watu wenye kutubu, watakatifu ambao wanataka kujua sauti ya Mungu!

Mlango unaoelezewa katika mstari wa ishirini unawakilisha ahadi - ambayo Wakristo wengi bado hawajafanya kikamilifu. Unaomba kwa Mungu na kuomba ushauri na uongozi lakini anataka zaidi! Anataka urafiki wako, hisia zako za kina. Anataka kukaa pamoja nawe na kushiriki kila kitu kilicho moyoni mwake.

Yesu amesimama kwenye mlango akigonga, akikualika ufungue mlango. Anaomba kujitolea kwa imani ambayo inasema utamufungulia Yesu moyo wako, roho yako na akili yako. Katika uwepo wake, jifunganiye ndani pamoja naye, utamjua. Na utajifunza kujua sauti yake - sauti ya yule anayependa vya kutosha kwa kugongagonga.