BABA YAKO ANASHIKILIA AHADI ZAKE

David Wilkerson (1931-2011)

Gethsemane ilikuwa ni bustani ambako Yesu alikwenda kuomba wakati kesi yake ilipoibuka na kikombe chake kilipomshinda. Ndio pale aliliaa kwa huzuni zake za kina mbele ya Baba. Na pia ni pale ambapo alishinda vita juu ya kila uovu na nguvu.

Wakristo wengine leo wanasema, "Kizazi chetu sio chenye machozi. Tumeitwa kusherehekea na kuamuru kuchukua kila kitu kwa imani. Tunaweza kusema Neno na kila mlima ukahamishwa. Tunapaswa tu kutafakari juu ya uzuri wa Mungu." Hiyo ndio mkao wa kanisa la kisasa la mafanikio.

Nakubali kwamba Mungu wetu ni Mungu wa upendo, ndiyo, tunapaswa kusherehekea mbele zake. Lakini kuna wakati ambapo majaribio yetu ni makubwa sana kwamba hatuwezi kufanya kitu lakini tu kuliliya mbele ya kiti chake cha enzi. Ilitokea kwa Yesu, lakini hakufanya dhambi katika kutokuamini wakati alipokuwa akiomba Gethsemane. Kinyume chake, Yesu alikuwa akiwaonyesha watu wake jinsi ya kupata nguvu na mamlaka juu ya nguvu zote za kishetani.

Fikiria maombi ya Yesu huko Gethsemane:

  • "Roho yangu inahuzuni nyingi kiasi cha kufa" (Mathayo 26:38). Azimio lake linasema, kwa kweli, "Hii ni zaidi ya ufahamu na ikiwa itaendelea, itaniua."
  • Yesu aliendelea, "Ee Baba yangu, ikiwa inawezekana, kikombe hiki kiniepuke" (26:39). Je! Umewahi kuomba katika huzuni sana adi machozi ya moto anakuja usoni mwako?

Yesu aliomba "sala ya mwisho" huko Gethsemane, maana ya sala ya mwisho ambayo ingeweza kusonga milima na kuitingisha kuzimu. Ilikuwa tu hii: "Si kama mimi nitakavyo, bali kama unavyotaka." Huenda umekuwa ushindana katika sala juu ya hali. Unamwambia Mungu jinsi ulivyofunga na kuombea, kugonga, kutafutwa na kuaminiwa, na hata hivyo vyenye unataka havikufika. Hii imeunda mgogoro halisi katika roho yako.

Ninakuhimiza kutupa kila kitu mikononi mwake na kuingia mahali pa kupumzika alipo andaa (Waebrania 4:1). Ameahidi, "Mimi nitakuwa Baba yenu, nanyi mtakuwa wana wangu na binti" (2 Wakorintho 6:18). Na Baba yako anashikilia ahadi zake!