"ACHA MDHAIFU ASEME 'MIMI NI HODARI'"

David Wilkerson (1931-2011)

Sisi sote tuna hatia ya kutokuamini wakati mwingine. Mara nyingi tunakabiliwa na jitihada nyingine na kuruhusu adui kutukatisha moyo. Tunapaswa kuendeleza hisia za upweke zisio na maana, au tunapoona hisia ya kutostahili jumla, tunaamini kuwa Bwana hatusikilizi. Kilio kinachimbuka kutoka mioyoni mwetu, "Mungu, uko wapi? Ninaomba, ninafanya toba, ninajifunza Neno lako. Kwa nini hauwezi kuniokoa kutoka kwa haa?"

Tunakwenda mahali penye siri kwa ajili ya maombi, lakini hatujisikia kama tunaomba. Roho zetu ni kavu, ziko bule, zimechoka kutokana na mapambano yetu. Hata hivyo hatuwezi kuthubutu kumshtaki Bwana kwa kutojali hali yetu. Kwa hiyo tunamkaribia tu katika kile tunachokiona kama unyenyekevu. Kichwa chini, tunasema kwa kukata tamaa, "Bwana, sikulaumu. Wewe ni mwema na unanifaa. Nina tatizo; Nimeshindwa sana."

Subiri! Hiyo siyo unyenyekevu. Kwa kinyume chake, ni kupoteza mwelekeo wenye kuwa wazi kwa Baba ambaye alituchukuwa kwa ahadi ya agano la kupenda na kutusayidia kupitia maisha yetu yote. Wakati tunamwambia jinsi tulivyo wabaya - udhaifu gani tunao, na kutofaa tunao mbele yake - tunadharau yote ambayo ametimiza ndani yetu. Hii inahuzunisha Baba yetu wa mbinguni.

Wakati wowote tunapofadhaika katika imani yetu, Roho Mtakatifu atasema nasi bila ya wusemi wa kwamba hakuna uhakika. "Huruma hii inakutosha. Simama! Unapendwa, uliitwa na kuchaguliwa, na nimekubariki kwa Neno langu. "Tunapaswa kujiadhibu ili tukumbuke yote ambayo Mungu ametuletea. Tunapaswa kufurahi, na kujua kwamba anafurahia kile alichotutendea.

Huenda ukajaribiwa mara kwa mara. Sasa wakati umekuja wa kufanya uamuzi. Mungu anataka imani inayovumilia mtihani wa mwisho, na anakupa Neno lake ili kukuwezesha kushinda. Ikiwa anakuagiza kufanya kitu fulani, atakupa nguvu na uwezo wa kumtii: "Acha aliye dhaifu aseme, 'Nina nguvu'" (Yoeli 3:10). "Muzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake" (Waefeso 6:10).