​KUSUBIRI SIKU YA UTUKUFU

David Wilkerson (1931-2011)

"Msifadhaike mioyoni mwenu; amini Mungu, na mimi pia muniamini. Nyumbani kwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningeliwambia; maana naenda kuwaandalia mahali kwa ajili yenu" (Yohana 14:1-2).

Wengi wetu wamehamisha hesabu ya mida kupitia maisha yetu,  lakini wakati tutapofika mbinguni, hatutahama tena. Yesu anatuambia kwamba amekwenda kutuandalia mahali na ni nyumba ya kudumu. Mwanamke Mkristo aliuliza, "Ikiwa mbinguni kutakuwa mengi asiewezekana kuhesabiwa, Mungu atawezaje kufanya makawo ya kila mtu? Inawezekanaje kuwa na nafasi ya kutosha kwa maeneo mengi?"

Hebu tuangalie maneno ya Yesu juu ya suala hili: "Naenda kuwaandalia mahali kwa ajili yenu" Maneno haya yanaoneka akimanisha kitu kwa ajili yetu. Baadhi ya wasomi wa Biblia hutafsiri maana ya Yesu hapa kama "makao mengi." Hiyo inaweza au si sahihi, lakini najua hili kwa uhakika: Ikiwa Yesu anajenga, tunaweza kuwa na uhakika kama ni kitu cha utukufu!

Unapochunguza mahali ambapo Bwana wetu anaandaa kwa ajili yako, usione picha ya majengo ya matofali au kitu kama hicho. Badala yake, makao yake ni ya eneo lingine kabisa. Kama wanadamu waliopangiwa mpaka, hatuwezi kufikiria eneo ambalo mwili hupita kwa kupitia vitu vyote vya kimwili ambavyo huonekana kama havikamiliki. (Yesu alifanya hivyo baada ya kufufuka kwake, na anasema kwamba mbinguni miili yetu itayopewa ukufu itakuwa kama yake.) Hapa ni eneo ambapo hakuna mwanasayansi ajawahi kupagundua, moja ya wingi watofauti kabisa ya kitu chochote tunachoweza kuelewa.

Jambo muhimu zaidi ambalo Yesu hufanya kuhusu mbingu ni, "Hii ni nyumbani! Wewe utaenda kuishi milele ambapo mimi naishi." "Basi mimi nikienda na kuaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo" (14:3). Shikilia tu, kuna nyumba ndani ya milele kwa kila mmoja wetu. Yesu alisema, kwa kweli, "Wakati siku hiyo itakapokuja - wakati utakapokuwa pamoja nami - nitakuonyesha mwenyewe kile nilichojenga kwako." Kweli, hiyo itakuwa ni utukufu!