​INGEKUWAJE KAMA TUNGEKUWA KANISA UMOJA?

Nicky Cruz

Baada ya Roho Mtakatifu kuzaa kanisa mal aya kwanza, na kuwatia wafuasi wa kwanza wa Yesu moto wake mtakatifu, matokeo ya haraka katika maisha yao yalikuwa makubwa na yote yaliyozunguka.

"Wakawa akidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali. Kila mtu akaingiwa na hofu; ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mitume. Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika, wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja. Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, makimega mkate nyumba kwa nyumba na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe, wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa" (Matendo 2:42-47).

Ninatamani kanisa la aina hii leo - mwili wa umoja wa Kristo. Na ninaamini Mungu anatamani hii pia. Hili ni kanisa linalounganishwa na maono wazi ya ujumbe wetu wenye kulazimisha katika ulimwengu huu. Ni kanisa lililounganishwa pamoja, kama waumini kila mahali kujifunza kuona watu waliopotea karibu nao kama Mungu anavyowaona. Na ni kanisa ambalo linashirikiana na roho hizi zilizopotea, ujumbe rahisi, unaojumuisha - habari njema ya Yesu Kristo.

Waumini wa karne ya kwanza walianza katika chumba kidogo na watu wachache tu, lakini walichukua changamoto hiyo, na Mungu alitumia uaminifu wao kufanya athari ya milele kwa utamaduni wao na dunia. Watu wa Mungu sasa ni idadi ya mamia ya mamilioni ulimwenguni kote, na kwanini hatuwezi kuwa na uwanja mmoja wa ujumbe, sisi sote tuna amri sawa kutoka kwa Yesu - kuhubiri ulimwengu.

Hebu fikiria kile kinachoweza kukamilika wakati watu wake wakienda pamoja ili kufikia waliopotea. Na unaweza kuwa sehemu ya mamlaka hii takatifu kwa kuwafikia wale walio karibu nawe - familia yako, wafanyakazi wenzako, majirani zako.

Nicky Cruz, mwinjilisti wa kimataifa aliyejulikana na mwandishi mkubwa, alimgeukia Yesu Kristo kutoka kwenye maisha ya vurugu na uhalifu baada ya kukutana na David Wilkerson huko New York City mwaka 1958. Hadithi yenye kushangaza  ya kuokoka kwake ilisemwa mara ya kwanza katika Musaraba na Kisu kinachomoka ( Cross and Switchblade) na David Wilkerson na kisha baadaye katika kitabu chake chenye kuuzwa vizuri zaidi, kiitwaco:Kimbiya , Mtoto, Kimbiya (Run, Baby, Run).