Mungu Hatawahi Kamwe Kuwaacha Watu Wake
Kwa kuwa BWANA huwapenda wenye haki naye hatawaacha waaminifu wake. Watalindwa milele, lakini uzao wa waovu utakatiliwa mbali, (Zaburi 37: 28).
Katika kitabu cha Luka 22, Yesu atoa Onyo kali sana kwa mfuasi wake mkuu. Yesu alimwita Mtume Petero kando na kumueleza kinaga ubaga: ““Simoni, Simoni, sikiliza, Shetani ameomba kuwapepeta ninyi wote kama ngano. Lakini nimekuombea wewe Simoni ili imani yako isishindwe…” (Luka 22: 31 – 32).
Najua Kwa Hakika
“Ninamjua Yeye niliyemwamini na kusadiki ya kuwa anaweza kukilinda kile nilichokiweka amana Kwake hadi siku ile. (Timotheo wa Pili 1:12, my italics). Haya ni maneno ya mtu aliyekuwa mwisho wa maisha yake, Mtume Paulo alikuwa akimueleza mwanafunzi wake, Mtumishi mchanga aliyekuwa mafunzoni, Timotheo. Katika barua hii, Paulo alimnong’onezea Timotheo maneno haya mazito. “Nimevipiga vita vizuri, mashindano nimeyamaliza, imani nimelinda” (Timotheo wa Pili 4:7). Ingawa Paulo aliamuandikia Timotheo, maneno haya yana umuhimu kwa kila Mkristo anaye pitia mateso.
Maneno ya Kutuliza Yenye Matumaini
Yesu alikuwa akihutubia umati mkuu pale ambapo watu walianza kuwa na njaa. Alimtwaa mtume Filipo na kumuuliza swali muhimu. “Yesu alipotazama na kuuona ule umati mkubwa wa watu ukimjia, akamwambia Filipo, “Tutanunua wapi mikate ili watu hawa wale?” Aliuliza swali hili kumpima, kwa maana alishajua la kufanya (Yohana 6:5–6). Yesu alikuwa akisema, “Filipo, maelfu ya watu wana njaa. Niambie, tutawalisha namna gani?
Habari ya Dharura
Nimeguswa na Roho Mtakatifu niwatumie ninyi nyote mulioko kwa mtandao wetu, kwa marafiki na maaskofu wale tumewahi kukutana kote Duniani.
JANGA KUU LITAKALO TIKISA DUNIA NZIMA LIKO KARIBU KUTOKEA. LITAKUWA LA KUTISHA SANA, SOTE TUTATETEMEKA - ATA WALE WANAO MUHOFU MUNGU KATI YETU.
Jeshi La Mungu Lililofichwa Nyakati Hizi Za Mwisho
Kuna jambo la ajabu duniani leo! Mungu yukazini anatenda jambo kwa Ukimya mafichoni – jambo lakimiujiza, binadamu hawawezi kulitafakari. Walakini, jambo hilo litatikisa dunia nzima nyakati hizi za Mwisho. Mungu anatayarisha Jeshi dogo la nguvu kati ya Wakristo! Jeshi hili ndilo litakuwa makini mno dunia nzima na Mungu atakuja kuwaongoza kutenda maajabu na kutingisa kuzimu. Mungu atamaliza nyakati akiwa na Jeshi Mabakio walio Makini na wasio na Uoga.
Watu Wa Mungu Hawata Aibika Katika Nyakati Za Janga Kuu
Nilipokuwa nikiliandaa neno hili, Gazeti la Wall Street Journal lilinakili kwamba Dunia nzima imefunikwa na wingu kuu la Uoga. Watu kutoka mataifa yote sasa wamebutwaa na matukio yalio ulimwenguni leo. Mara moja nilianza kuwaza kuhusu waumini wa hapa kwetu Times Square Church. Hawana uoga kama huwo. Ingawa tumemakinika na matokeo hayo, tuko pia na Furaha kuu. Nikaongozwa pale kwa Zaburi 37, ilioandikwa na Daudi: “BWANA anazifahamu siku za wanyofu, na urithi wao utadumu milele. Siku za maafa hawatanyauka, siku za njaa watafurahia kuwa na wingi wa vitu.
Wakati Wa Kilio na Wakati wa Vita
Nisomapo Agano la Kale, Imani yangu hupata nguvu na ule mfano wa Daudi. Jambo baya lilikuwa limemfanyikia mtu huyu, mpaka maisha yake yalikuwa yametishwa na wale waliokuwa wandani wake. Ninajengwa Imani na vile Daudi alivyo tafuta neno kutoka kwa Mungu wakati huu wa shida kuu. Ilikuwa hivi: Daudi pamoja na majeshi yake 600 walikuwa wanamtoroka Mfalme Sauli aliyakuwa akitaka kuwaua. Walifika mahali paitwapo Siklagi wakapiga kambi pamoja na familia zao. Kisha wakaenda vitani mabibi na watoto wakiwa wamebaki hapo kambini.
Wako Wapi Wale Wengine Tisa?
Tafakari tukio hili kutoka Luka 17: Yesu alikuwa akielekea Yerusalemu wakati kusulubiwa kwake kulikuwa karibu. Alipokuwa akipita katikati ya Samaria na Galilea, alikaribia kijiji fulani ambapo kulikuwemo Wakoma kumi nje ya kijiji hiki waliokuwa wamepiga kambi kwa uchungu na pia aibu kuu. Kwa kweli, tisa kati ya hawa Wakoma kuni walikuwa wayahudi na mmoja aklikua Msamaria. Kumbuka kwamba, Wayahudi wa siku hizo walikuwa hawawezi hata kuwagusa Wasamaria wacha hata kuishi nao. Yaonekana shida ya ukoma iliyowakumba watu hawa iliwalazimu kubeba pamoja shida hii ya Ukoma.
Ameyapaka Macho Yao Ndiposa Wasiweze Kuona
“Wote wachongao sanamu ni ubatili, vitu wanavyovithamini havifai kitu. Wale ambao wangesema juu yao ni vipofu, ni wajinga, ili wao waaibike. Ni nani atengenezaye mungu na kusubu sanamu, ambayo haiwezi kumfaidia kitu cho chote?


ShareThis