Sermons  Pulpit Series Newsletters   Habari ya Dharura

Habari ya Dharura

Janga Kuu liko karibu kutokea Ulimwenguni

by David Wilkerson | March 7, 2009

ShareThis   Print  Print

March 7, 2009

Nimeguswa na Roho Mtakatifu niwatumie ninyi nyote mulioko kwa mtandao wetu, kwa marafiki na maaskofu wale tumewahi kukutana kote Duniani.

JANGA KUU LITAKALO TIKISA DUNIA NZIMA LIKO KARIBU KUTOKEA. LITAKUWA LA KUTISHA SANA, SOTE TUTATETEMEKA - ATA WALE WANAO MUHOFU MUNGU KATI YETU.

Kwa miaka kumi sasa nimekuwa nikiwaonya kuhusu Mioto elfu moja ya New York City, itakayo funika megacomplex yote, mpaka New Jersey na Connecticut. Migomo na Misukosuko ya watu itazuka katika miji mikuu hapa Amerika – kama yale ya Watts, Los Angeles miaka iliyopita.
Misukosuko ya watu na mioto itaikumba miji ya Ulimwengu. Kutakuwa na kuporwa kwa mali – hata hapa kwetu Times Square, New York. Yale tunayo yaona leo sio tu kudhoofika kwa Uchumi. Tuko katika Hukumu ya Mungu. Imenakiliwa katika Zaburi 11:3

“Wakati misingi inapoharibiwa, mwenye haki anaweza kufanya nini?’’
Mungu anahukumu dhambi za Waamerika na za Dunia yote. Anaivunja misingi ya Kidunia.

Nabii Yeremia aliwasihi waisraeli walipokuwa wamemuasi Mungu, ‘‘Basi kwa hiyo waambie watu wa Yuda na wale waishio Yerusalemu, ‘Hili ndilo asemalo BWANA: Tazama! ninaandaa maafa kwa ajili yenu nami ninabuni mabaya dhidi yenu. Kwa hiyo geukeni kutoka katika njia zenu mbaya, kila mmoja wenu, tengenezeni njia zenu na matendo yenu.’ Lakini wao watajibu, ‘Hakuna faida. Tutaendelea na mipango yetu wenyewe, kila mmoja wetu atafuata ukaidi wa moyo wake mbaya.’’ Yeremia 18:11-12)

Katika Zaburi 11:6, Daudi anaonya, “Juu ya waovu atawanyeshea makaa ya moto mkali na kiberiti kinachowaka, upepo wenye joto kali ndio fungu lao.” Na ni Kwanini? Daudi ajibu, “Kwa kuwa BWANA ni mwenye haki, hupenda haki”. Hili ni tukio la Hukumu ya Haki Kutoka kwa Bwana Mungu kama alivyofanya Sodom katika kizazi cha Noah.

WATAKATIFU WATAFANYA NINI? ITAKUWAJE KWA WATU WA MUNGU?

Jambo la kwanza ni hili nililopokea kwa makusudi yangu mwenyewe, tenga kando kiwango cha siku 30 cha chakula isiyoweza kuharibika, vitu vya bafuni na choo na vitu muhimu. Katika Miji mikuu ulimwenguni, vitu hivi vitapotea madukani kwa upesi mno kunapotarajiwa Janga kuu.

Kiroho, tuko na njia mbili. Zimenakiliwa katika Zaburi 11:1 “Ruka kama ndege kwenye mlima” Au kama asemavyo Daudi, “BWANA yuko ndani ya hekalu lake takatifu, BWANA yuko kwenye kiti chake cha enzi mbinguni Huwaangalia wana wa watu, macho yake yanawajaribu. (mstari wa nne). “Kwa BWANA ninakimbilia” (mstari wa kwanza).

Nita ambiya Nafsi yangu: Hamna haja ya kutoroka...hamna haja ya kujificha. Hili ni tukio la Haki kutoka kwa Mungu. Nitamtegemea Mungu aliye katika Kiti chake cha Enzi, macho yake ya Upendo na huruma yakitazama mienendo yangu – nikiamini ya kwamba atakomboa watu wake hata kutoka kwa Mafuriko, Mioto, Janga na Majaribu ya aina yote.

Zingatia: Sijui mambo haya yatatendeka lini, lakini najua hayako mbali sasa. Nimeeleza yote yale yaliokuwa mzigo katika Nafsi yangu. Fanya na habari hii vile utakavyo chagua wewe mwenyewe.

Mungu akubariki na akulinde.

Katika Kristo
DAVID WILKERSON

Vizuizi vya Hakimiliki/Uvyazi: Data hii/uchapishaji huu ni mali ya World Challenge, Inc. Inaweza kuchapishwa kwa ukamilifu kwa matumizi ya wasomaji pekee au pamoja na familia na marafiki. Haipaswi kugeuzwa au kuharirishwa kwa njia yeyote ile na Uvyazi wa data hii/uchapishaji huu lazima iwe na Notisi hii ya Hakimiliki. Data hii sio ya kutumwa au kuchapishwa wazi kwa Mtandao au FTP ila katika Mitandao ya worldchallenge.org, davidwilkerson.org au tscpulpitseries.org

© 2009 World Challenge, Inc., PO Box 260, Lindale, Texas 75771


  Back to Top